MKASIMAMIE UCHAGUZI KWA KUZINGATIA SHERIA – KIGAILE

Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi Jimbo la Kahama, wametakiwa kuzingatia sheria wakati wa zoezi la uchaguzi, ili kutenda haki na kufanya uchaguzi kuwa huru na amani.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo kwa wasimamizi hao, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kahama, Sadick Kigaile amewataka kuzingatia kanuni zinazowaongoza na kuvishirikisha vyama vyote vya siasa kila hatua ili kuondoa malalamiko wakati wa uchaguzi.

“Simamieni haki na kanuni za uchaguzi ,haya mafunzo mliyopewa hapa yakawe mwanga katika usimamiziwenu lakini pia washirikisheni vyama vyote za siasa katika kila hatua ili kuoandoa malalamiko wakati wa Uchaguzi” Amesema Kigaile.

Kwa upande wake Afisa kutoka Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi, Furaha Thomas amewataka Watendaji hao kuzingatia mafunzo na watambue kuwa jukumu walilopewa kwasasa wao wako chini ya tume ya uchaguzi hivyo ni vyema kufuata misingi ya tume.

“Niwaombe zingatieni sana mafunzo mnayopewa kwani ndo mwongozo utakaowasaidia kusimamia vyema uchaguzi,lakini hili jukumu mlilopewa nyinyi sasa mnakuwa upande wa tume hivyo ni vyema kufuata misingi na miongozo ya tume”Amesema Thomas.

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamehaidi kusimamia vyema misingi ya Tume ya Uchaguzi na kuwa waadilifu wakati wote wa zoezi la uchaguzi na kutumia vyema mafunzo waliopatiwa.

“Tunashukuru sana kwa mafunzo haya na sisi tunahaidi kusimamia vyema misingi ya tume ya uchaguzi na tutakuwa waadilifu wakati wote wa zoezi  hili kwa kutumia mafunzo haya tuliyopatiwa,” wamesema watendaji hao.

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imeendelea kufanya mafunzo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi huku takribani wasaidizi 40 kutoka kata 20 za Manispaa ya Kahama wakishiriki mafunzo hayo ya siku tatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *