MKANDARASI AHIMIZWA UKAMILIFU WA MIRADI KWA WAKATI KIGOMA

Na Tryphone Odace – Kigoma.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho, amemtaka mkandarasi anayejenga Soko la Mwanga, Mwalo wa Katonga na Bwawa la Katubuka katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, Mkoa wa Kigoma, kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati.

Waziri Nyansaho ametoa agizo hilo leo Agost 24, 2026, wakati akiendelea na ziara yake mkoani Kigoma, yenye lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya kimkakati. Amesema kukamilika kwa miradi hiyo kutasaidia kurahisisha upatikanaji wa huduma na kuchochea shughuli za kiuchumi kwa wananchi.

Alisema miradi hiyo ni ya kimkakati na lengo la Serikali ni kuufungua mkoa wa kigoma na tusopofanya haraka kipindi cha mvua kimekaribia kwahiyo tunaweza kukwamishwa na kutofikia malengo.

Akizungumza katika ziara hiyo, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Zainab Katimba, alisema dhamira ya Serikali ni kuhakikisha Mkoa wa Kigoma unakuwa kitovu cha uchumi kwa Kanda ya Magharibi.

“Kukamilika kwa soko hili na miradi hii yote ni sehemu ya kuendelea kuboresha huduma kwa jamii ya kigoma na taifa kwa ujumla”Alisema Katimba

Naye Mkandarasi wa miradi hiyo, Mha. Joseph John Marandu, akitoa ufafanuzi kuhusu thamani ya miradi hiyo na manufaa yatakayopatikana mara itakapokamilika.

Aidha, katika hatua nyingine ya ziara hiyo, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho, ametembelea na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS), Tawi la Kigoma.

Ujenzi wa chuo hicho umefikia asilimia 99.71, hatua inayokaribia kukamilisha mradi huo na kuwezesha wananchi wa Mkoa wa Kigoma na maeneo ya jirani kunufaika na huduma za elimu ya afya pamoja na kuongeza fursa za mafunzo katika kada mbalimbali za afya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *