Jambo La Leo

Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Mitandao mitano inayotumika zaidi Afrika

Mtandao wa Business Insider, umetaja orodha ya mitandao mitano ya kijamii inayotumika sana kwa mwaka huu 2023.

Katika mitandao hiyo kuna mitandao wa Facebook huu ndio wa kwanza kutumika sana Afrika ambapo unawatumiwa na watu wapatao Milioni 170 sawa na 82% ya watu wote. Ila 68% ya watumiaji ni wale wanaotumia kwa matukio maalumu na 49% wapo hapo kutengeneza marafiki wapya.

Mtandao unafuata kuwa na watumiaji  wengi ni Tik Tok, ambapo 61% ndio watumiaji, ila  73% utumia kutazama na kushiriki video fupi. Na 72% wanaiona kama chanzo cha kupata burudani na video za ucheshi.

Mtandao mwingine ni Instagram, wenyewe unajumla ya watumiaji 54%, kali ya yote kuna 62% wanatumia Instagram kama sehemu ya kupata mawazo mapya ya ubunifu. Na kuna wale wanowafuatilia watu maarufu tu na wenye ushawishi, watu hawa wapo 61% na 59% wapo kwenye mitandao huu kuweka picha na video zao kama sehemu ya kumbukumbu.

Huu ulizua taharuki sana ulipobadilishwa jina kutoka Twitter hadi X, wenyewe unawatumiaji 49% ambapo wanatumia mitandao huu kama chanzo cha habari. Kuna 78% ni watumiaji wa zamani na wengi wao ni wale wanaotafuta habari hasa waandishi wa habari, ila 59% ni wale ambao wanatumia mitandao huo kama sehemu ya kuanzisha na kuibua mijadala.

Reddit  ni wa tano ambapo unaweza kuwa na 6% ya watumiaji barani Afrika, lakini athari yake ni ya kushangaza. Miongoni mwa watumiaji hawa, 75% hujadili kikamilifu mambo mahususi yanayokuvutia au mambo ya kupendeza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *