Na Afarah Suleiman, Babati – Manyara.
Serikali mkoani Manyara, imezindua mradi wa uchimbaji wa visima 40 katika Vijiji 40 vya Wilaya tano za mkoa huo kwa lengo la kufikia malengo ya Agenda 10/30, kuongeza usalama wa chakula na nakuleta kilimo chenye tija ndani ya mkoa huo.
Mitambo hiyo imezinduliwa leo Oktoba 23, 2025 na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga na kuwataka Maafisa Kilimo kuweka mpango maalum wa kuwafikia Wakulima na kuwaeleza juu ya Dalila za awali za magonjwa ya mazao, kabla ya kuleta madhara makubwa kwenye mazao ya Wananchi.

Kwa upande wake Mhandisi Umwagiliaji Mkoa wa Manyara, Richard Mgaya amesema visima hivyo vitachimbwa katika Wilaya zote tano za mkoa huo ambapo Wilaya ya Babati itakuwa na visima 12, Wilaya ya Hanang’ visima vitano, Wilaya ya Mbulu visima 10, Wilaya ya Simanjiro visima vitano na Wilaya Kiteto visima nane.
Nao Baadhi ya wananchi waliofika kwenye uzinduzi huo, wameishukuru serikali kwa kuwaletea mradi wakisema utakwenda kuwarahisishia upatikanaji wa Mboga mboga na Matundakupitia Kilimo cha umwagiliaji.



