Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Miss Tanzania akabidhiwa Bendera kuiwakilisha nchi,Miss world

Mshindi wa Mashindano ya ulimbwende nchini (miss Tanzania) Halima Kopwe mapema leo amefika BASATA  na kukutana na Katibu mtendaji Dkt. Kedmon Mapana.

Baada ya kufika BASATA  Katibu Mtendaji  Mapana amemkabidhi Bendera kwa ajili ya kwenda kuiwakilisha nchi katika mashindano ya dunia ya Ulimbwende (Miss world) nchini India.

Aidha Bi.Halima Kopwe amehaidi kuipeperusha Bendera ya Nchi vyema kwani amesema kuwa amejipanga vizuri katika kushiriki mashindano hayo.

Nae Katibu Mtendaji Mapana amemtakia kila la kheri katika mashindano hayo na kusema kuwa Taifa liko pamoja katika kumpa ushirikiano utakapohitajika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *