MISAADA INAPOTOLEWA IWAFIKIE WALENGWA – DC NAANO

Na Saada Almasi, Maswa – Simiyu.

Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Vicent Naano amewataka wazazi na walezi ambao wanaishi na watoto wanatoka katika mazingira magumu kuhakikisha wanafikisha na kutumia misaada wanayopewa na wadau mbalimbali kutimiza makusudio yaliyotazamiwa.

Naano amebainisha hayo wakati wa kukabidhi msaada uliotolewa na kanisa la TAG Ebeneza lililopo mtaaa wa Majengo wilayani humo kwa watoto 215 walio katika mazingira magumu wilayani humo na kusema kuwa haitokuwa sawa kama misaada hiyo haitowafikia walengwa.

“Unapopokea msaada basi jua kuwa huo ni masaada kwa nini walete kwako wakati kuna wengine wenye uhitaji? na hawa waliotoa si kwamba ni matajiri sana hapana ni moyo wa upendo walionao ukawafanya wafike kwako hivyo niwaombe isitokee watoto wanalala chini halafu kitanda cha msaada amelalia mtu mzima,chakula kizuri anakula mtu mzima halafu mtoto apunjwe haitokuwa sawa,kila mlichopokea kifike kwa mlengwa,” amesema Naano.

Msaada huo, umetolewa wakati baadhi ya wakazi wa wilaya hiyo wakilala chini na kukosa mahitaji muhimu kama chakula na mavazi wakisubiri watanzania wenye huruma kuwatizama ndipo kanisa hilo likaona vema kuwakusanya wahitaji wao na kuwapatia msaada wa vitu mba;imbali vyene thamani ya shilingi milioni 30.

Mchungaji wa Kanisa hilo, Enock Sumaye amesema kuwa walipata wazo la kiusaidia watoto kutoka mazingira magumu 50 kutoka wilaya hiyo na sasa wamefikisha watoto 215 ambao licha ya kuwapatia mahitaji ya malazi na chakula pia wanapata elimu.

“Hiki kituo kinafanya kazi na washirika wenza shirika la Compassion International Tanzania ambaapo awali tulianza na watoto 50 kuwahudumia lakini sasa tumefikisha watoto 215 na kati yao wapo wadugo wa chekechea na shule ya msingi ambao tunaendelea kuwapa elimu na kuwahudumia,” alisema Mchungaji Enock.

Jambo Fm imezingumza na baadhi ya wanufaika wa msaada huo ambao wamekiri kupokea huku ewakiwataka kuendelea kusaidia watu wengine zaidi.

“Tunaishi mazingira magumu sana wengine tunalala chini hatuna njia yoyote ya kununua hata magodoro lakini sasa tumepewa,nashukuru Mungu kwa ajili yenu kutuletea msaada huunaomba muendelee kutoa ili msaidie na wengne,“ alisema Shida Idd.

“Nimekuwa katika wakati mgumu sana kwa muda mrefu hili kanisa waliniona wakanichukua na kunipa msaada hawakujali imani yangu bali kunisaidia kutoka kwenye hali yangu ngumu,nawashkuru sana sasa hivi nimepata godoro  watoto wangu watalala vizuri ni nitawafikishia,” amesema Mwanaidi Juma.

Msaada uliotolewa ni pamoja na vitanda 50,magodoro 66 vyandarua 215 sambamba na vifaa vya kujisomea yakiwemo mabegi ya shule na nguo za mazoezi  kwa wanafunzi ambao bado wapo shule na kuweka jumla ya gharama ya Shilingi Milioni 30,300,000.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *