MIRADI YA UMEME PEMBEZONI MWA MIJI KUWANUFAISHA WAHITAJI

Na Gideon Gregory – Dodoma.

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema maeneo ambayo wananchi wanapata tabu kuunganishiwa umeme kwakuwa uchumi wao ni wa chini, Serikali inayo mikakati ya kuweka miradi ya pembezoni mwa miji ili wananchi waunganishiwe huduma hiyo kwa bei rahisi. 

Naibu Waziri Kapinga ameyasema hayo leo Aprili 11,2025 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Christina Mzava kwa niaba ya Mbunge wa Kishapu Boniphace Butondo aliyetaka kujua ni ipi kauli ya Serikali juu ya Kata ambazo hazijaunganishiwa umeme Kahama na Shinyanga. 

Amesema”kwa maeneo kama hayo pia tutayazingatia kwa kupeleka miradi hii na wananchi waweze kuunganisha umeme kwa elfu 27,000 kulingana na miradi ya pembezoni mwa miji,”.

Awali akijibu swali la msingi la Mhe. Butondo juu ya lini Vijiji 42 vilivyobaki vya Wilaya ya Kishapu vitapatiwa umeme, Kapinga amesema Jimbo la Kishapu lina jumla ya vijiji 117 ambapo hadi kufikia tarehe 30 Machi, 2025 vijiji vyote 117 sawa na asilimia 100 vilikuwa vimekwisha unganishwa na huduma ya umeme kupitia miradi mbalimbali iliyotekelezwa na Serikali. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *