MILIONI 63 ZATOLEWA KWA VIKUNDI 10 VYA WAJASIRIAMALI KIGOMA.

Taasisi ya CRDB Bank Foundation kwa Kushirikiana na Manispaa ya Kigoma Ujiji imetoa hundi ya kiasi cha shilingi Million 63 kwa vikundi kumi vya wanawake Wajasiriamali ikiwa ni ni utekelezaji wa utolewaji wa mikopo kwa makundi ya Wanawake Vijana na watu wenye Ulemavu itokanayo na asilimia kumi ya Mapato ya ndani.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Kigoma wakati wa kukabidhi hundi hiyo Katibu wakati wa wilaya hiyo Mganwa Nzota amevitaka vikundi hivyo kurejesha mkopo huo kwa wakati na kwa uaminifu ili uweze kuwanufaisha na vikundi vingine

“Niwasihi sana ninyi ambao mmepata nafasi ya kupita katika hatua hii zingatieni sana uaminifu na nidhamu ya Pesa, tumieni mkopo huu kufanya shughuli mliyokusudia lakini mkumbuke kurejesha kwa wakati ili kutoa nafasi kwa watu wengine kukopa”Alisema Mganwa.

Naye Meneja wa CRDB Bank Foundation Tawi la Kigoma Fadhili Bushagama amesema baada ya Mapitio ya maombi juu ya vikundi vya wanawake vilivyoomba mkopo huo wamejiridhisha kuwa ni vikundi vinane pekee kati ya vikundi 18 vilivyoomba mkopo vimekidhi vigezo vya kunufaika na Mkopo huo 

Aidha Bushagama amesema wanaendelea kushirikiana na Maofisa maendeleo ya Jamii wilaya pamoja na viongozi wa Vikundi mbalimbali ili kuwasaidia kurekebisha Kasoro zinazowafanya kukosa sifa za kunufaika na Mikopo hiyo nafuu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *