Mikaratusi Kufanyiwa Utafiti Athari za Kimazingira

Serikali kupitia taasisi ya utafiti wa Misitu nchini(TAFORI) inaendelea na utafiti wa kina wa miti ya mikaratusi ili kuja na taarifa ya kitaalam pamoja na ushauri kuhusu athari za kimazingira ya aina hiyo ya miti.
Hayo yameelezwa leo Aprili 30,2024 Bungeni Jijini na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais ( Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis alipokuwa akijibu swali Mbunge wa Hai Saashisha Mafuwe aliyetaka kujua Serikali inatoa tamko gani kuhusu kuteketeza Miti ya Mkaratusi nchini baada ya tafiti kuonyesha ina haribu mazingira.
“Kwanza napenda kulifahamisha Bunge lako Tukufu kwamba si kila Mti wa Mkaratusi una athari kubwa kwenye Mazingira, kuna zaidi ya spishi 500 za miti ya mikaratusi duniani”, amesema.
Amesema Tanzania kupitia TAFORI imeruhusu aina 25 za mikaratusi ili kupata fursa mbalimbali zitokanazo na mikaratusi hasa kwenye viwanda vya mazao yaliyosindikwa (Engineered wood product).
Pia ameongeza kuwa mara baada ya tafiti kukamilika Ofisi ya Makamu wa Rais na Wizara ya Maliasili na Utalii zitatoa taarifa, pamoja na kutoa elimu kwa wananchi wote kwa ujumla.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *