MIGOGORO YA ARDHI KAHAMA KUKOMESHWA.

Migogoro ya ardhi katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga huenda ikafika kikomo baada ya kuanza kwa mradi wa Mpango Kabambe wa kidikitali (Master Plan) utakaotekelezwa mpaka mwaka 2050 ili kufanya Kahama kuwa mji wa kisasa na uliopangika.

Hayo yamesemwa na Mtaalam mshauri kutoka Kampuni ya Urban Solution Hamisi Mkoma wakati wa mafunzo kwa watendaji wa vijiji, kata na wenyeviti wa vijiji wa Manipaa ya Kahama ili kuanza kutekeleza mradi huo, ambapo amesema kwa kata 8 za vijiji zitabadilika katika sekta mbalimbali ikiwemo masuala ya ardhi, Mazingira, biashara, kilimo na mifugo.

“Mpango huu utaenda kubadili kabisa jina la maeneo yetu hasa katika kata 8 za vijiji na utakuwa na mabadiliko katika masuala ya ardhi,Mazingira biashara,kilimo na ufugaji” Amesema Mkoma.

Aidha, Mkoma amesema kuwa baada ya kukamilika kwa mradi huo Kahama itakuwa mji wa kisasa na wenye mpangilio mzuri hali itakayosababisha halmashauri nyingine nchini kuja na kujifunza ikiwa ni kwa mara ya kwanza kufanyika katika Manipaa hiyo.

“Kahama itakuwa mji wa kisasa kabisa na itafikia mahali halmashauri nyingine nchini zitakuja kujifunza Kahama na sasa ndo tunaanza kwa mara ya kwanza mpango huu kabambe wa kupanga manispaa hii” Ameongeza Mkoma.

Kwa upande wao, Afisa mtendaji wa kata ya Kilago Cosmas Bukango na afisa mtendaji wa kijiji cha Isagehe Amina Mgumba wamesema kuwa Mpango huo utasaidia kuondoa utapeli kwa baadhi ya watu wanoanzisha migogoro ya ardhi kwa kuwa na mifumo ya kidikitali itakayorahishia kuondoa migogoro hiyo.

“Kahama yetu imekuwa ya migogoro ya ardhi kila mahala sasa mpango utasaidia kuondoa Utapeli kwa baadhi ya watu ambao wamekuwa wakianzisha migogoro mara kwa mara” Wamesema watendaji hao.

Nao Baadhi ya wenyeviti wa vijiji wa Manispaa hiyo wamesema kuwa kuanza kwa mradi huo utapunguza migogoro ya ardhi,huku wakiomba serikali kushirikiana na wataalum kuendelea kutoa elimu juu ya badiliko katika sheria kabla ya kuanza kwa utekelezaji wa mradi huo.

“Hili swala ni zuri sana sasa tunaomba serikali kwa kushirikiana na wataalamu wandelee kutoa elimu juu ya mabdiliko haya katika sheria kabla ya kuanza kwa utekelezaji wake” Wamesema.

Mradi huo unatekelezwa katika kata 20 za Manispaa ya kahama, huku kata za kinaga, Isage, Mondo, Ngogwa, Nyandekwa, Kilago na Wendele zinabadilika kutoka kwenye vijiji na vitongoji kuwa mitaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *