MIGOGORO 9069 IMEIBULIWA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA TOKA IMEANZISHWA

Imeelezwa kuwa Kampeni ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia imesaidia na kuibua Migogoro na changamoto za kisheria Elfu 9 na 69 toka mwaka 2023 ilipoanzishwa ambapo kampeni hiyo imekuwa Mkombozi kwa wananchi kutatuliwa migogoro kisheria pamoja na kupewa elimu hiyo.

Hayo yameelezwa na Mwakilishi wa Naibu Waziri Mkuu ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Geita , Martine Shigela wakati akitoa taarifa ya Uzinduzi wa Kampeni ya utekelezaji ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia mjini Geita ambapo amesema toka kampeni hiyo imeanza tayari imewafikia wananchi zaidi ya Laki 779191 huku laki 3 na 89 wakiwa ni wanawake na wanaume wakiwa ni Laki 3 na 89.

“Ndugu zangu wananchi wenzangu kama mlivyosikia tangu kampeni hii imeanza imeweza kukava zaidi ya wananchi Laki saba na 79191kati yao Laki tatu na 89 ni wanawake Laki tatu na 96 ni wanaume kwahiyo hata sisi wanaume kama alivyosema na sisi tunayo matatizo mengi yanayotusumbua ,” Mwakilishi wa Naibu waziri Mkuu , Martine Shigela.

“Tunawapongeza sana wale wote ambao mmeweza kuifikia kazi hii ya kuwagusa watu zaidi ya Laki saba na 79 na kuibua Migogoro au changamoto za kisheria Elfu 9069 na katika hilo iliyotatuliwa na kupata suluhu ya kudumu ni zaidi ya Elfu moja 505 leo katika kampeni hii tunaenda kuongezeka kwenye Laki saba na 79 mara tutaelekea kwenye laki nane , ” Mwakilishi wa Naibu Waziri Mkuu , Martine Shigela.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wizara ya Maendeleo ya Jamii na Makundi Maalumu , Amon Mpanju amesema serikali ya awmu ya sita inayo ongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan imelenga kupeleka fedha za uwezeshwaji wananchi kiuchumi pamoja na wafanyabiashara ambapo kiasi cha shilingi Bilioni 10.5 kimetegwa kwa ajili ya kuwakwamua wananchi kiuchumi.

“Mambo mengine ya ukatili vipigo vya akina mama ni kwasababu watu hawajawezeshwa kiuchumi serikali ya awamu ya sita ya Mh Dkt.Samia Suluhu Hassan imelenga kupeleka fedha na uwezeshaji wananchi mpaka ngazi ya chini Mh kati ya maeneo tunayosimamia ni suala la upatikanaji wa mikopo kwa wafanyabiashara ndogo ndogo ,” Naibu Katibu Mkuu wizara ya Maendeleo ya Jamii na Mkundi maalumu , Amon Mpanju.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *