Migogoro 300 yawasilishwa Manispaa ya Shinyanga

Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia imeshughulikia migogoro zaidi ya 300 iliyohusisha mirathi,ardhi na ukatili wa kijinsia kwa hatua tofauti tofauti ilhali mingine ikihitaji hatua zaidi za kisera na kisheria ili iweze kufanyiwa kazi ndani ya Manispaa ya Shinyanga.

Mratibu wa kamati ya Ulinzi na Usalama wa wanawake Mkoa wa Shinyanga, Tedson Ngwale amebainisha hayo wilayani Kishapu wakati akizungumza kuhusiana mafunzo ya siku tatu ya kuzijengea uwezo kamati za Ulinzi na Usalama wa watoto ambazo pia zimepewa mafunzo kuhusiana na Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia.

Kupitia mafunzo hayo yaliyoendeshwa Idara ya Mipango na Uratibu ya Mkoa kwa Kushirikiana na Wildaf chini ya Ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya watu (UNFPA), kamati hizo zimeongezewa nyenzo zaidi zitakazotumika katika kuwasaidia wanahitaji huduma ya Msaada wa kisheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *