Mifuko ya plastiki bado ni tatizo

Leo Julai 3 ni siku ya Mifuko ya Plastiki Duniani, Juni Mosi mwaka 2019 Serikali ya Tanzania ilianza rasmi utekelezaji wa hatua ya kuachana na mifuko ya plastiki kwa kubebea bidhaa kuanzia nyumbani, madukani na hata masokoni.

Marufuku hiyo ilihusisha kuzalisha, kuagiza, kusafirisha nje ya nchi, kuhifadhi, kusambaza, kuuza, kumiliki na kutumia mifuko ya plastiki katika eneo lote la Tanzania bara.

Tanzania ilifuata nyayo za mataifa mengine ya Afika Mashariki ambayo ni Rwanda na Kenya ambayo yalitangulia kuanza utekelezaji wa makubaliano ya kimataifa ya kulinda mazingira dhidi ya bidhaa za plastiki.

Hali ya Matumizi ya mifuko ya Plastiki Duniani na Tanzania
Inakadiriwa kuwa, matumizi ya mifuko ya plastiki duniani ni bilioni 500 mpaka trilioni moja na nchini Tanzania, tani 350,000 ya mifuko ya plastiki huzalishwa kila mwaka ambapo hii ni chini ya asilimia kumi (10%) ya mifuko iliyotumika hurejereshwa(Chanzo Tovuti ya NEMC).

Aidha Kutokana na tafiti mbalimbali mifuko ya plastiki huchukua miaka 400 mpaka 1000 kuoza ardhini.

Miongoni mwa madhara ya matumizi ya mifuko ya Plastiki ni pamoja na Kuathiri mifumo ikolojia ya bahari ambapo Inakadiriwa 100,000 viumbe bahari na ndege bahari millioni moja kila mwaka wanakufa kwa kula mifuko ya plastiki).

Aidha mifuko ya plastiki huchafua miji kutokana na kushindwa kuoza,kuathiri mifugo (Mfano ranchi ya Kongwa mkoa wa Dodoma Ng’ombe 57 walikufa mwaka 2017 kutokana na kula mifuko ya plastiki.

Kuharibu miundombinu kwa kuziba kwenye mifereji na baadhi ya njia za maji pamoja na Kubeba na kusambaza viumbe vamizi na bacteria.

Kutokana na madhara ya mifuko ya plastiki, Serikali ilitoa tamko la kusitisha matumizi ya mifuko ya plastiki mnamo tarehe 1 Juni, 2019 na kuandaa Kanuni ya Usimamizi wa katazo la Matumizi ya Mifuko ya Plastiki iliyotoka kwenye Gazeti la Serikali Na. 394 (The Environmental Management (Prohibition of Plastic Carrier Bags) Regulation, 2019, which made under section 230 (2) (f) of the Environmental Management Act, Cap 191).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *