Na Cecilia Shiratu, Bukoba – Kagera.
Wazazi wametakiwa kuwaruhusu watoto na vijana wao kushiriki katika michezo, kwani hujenga afya njema , kuwapatia ajira na kuwaepusha vijana kuingia katika obwe la matumizi mabaya ya mitandao na kujikita zaidi kwenye michezo.
Wito huo, umetolewa na Afisa Mnadhimu Mkoa wa Kagera, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Yussuf Daniel ambaye alimwakilisha Kamanda wa Polisi mkoa wa kagera katika fainali za Mwijage CUP, zilizofanyika Kamachumu Wilaya ya Muleba na ambapo amemuomba Mkurugenzi na Mwandamizi wa mashindano ya Paul Mwijage Cup, kuanzisha pia timu za vijana wadogo, ili kuibua vipaji halisi vinavyopatika Kamachumu.

Mkurugenzi wa mashindano ya Paul Mwijage Cup alisema, yana lengo la kuinua vipaji vya vijana wa Kamachumu na watakaofuzu mashindano hayo watapatiwa nafasi ya kushiriki katika michuano mikubwa katika timu mbalimbali, ikiwemo Kagera Sugar na Geita gold.
Ameongeza kuwa, wataunda uongozi na katiba kupata timu ya kamachumu FC ambayo itakua ni timu ya wananchi ambayo wanatarajia kuipambania Ili ishiriki lingi kuu Tanzania Bara.

Naye Katibu itikadi Mwenezi na mafunzo wa CCM mkoa wa Kagera, Hamimu Mahamudu amewashukuru waandaji wa mashinda hayo kwa kuibua fursa ya ajira na kukuza vipaji vya vijana ili kupata wachezaji wakubwa kutoka Kamachumu kama vile Salum Ahmed Harufani, Adala Ahmedi Harufani, Wile kamugisha na Didas Zimbiile.



