Unakumbuka hapa juzi Cardi B wakati wa onyesho lake huko Las Vegas, alitumia mic/kipaza sauti kumtwanga shabiki aliyemwagia maji!! sasa kampuni ya kutengeneza sauti ya The Wave in Sin City, ambao ni wamiliki wa mic wameamua kuipiga mnada mic hiyo ili kusaidia jamii yenye uhitaji.
Kampuni ya eBay na Scott wameanzisha mnada wa mic kwa kiasi cha $500- $1,000 ila mpaka sasa inaelezwa imefika $94,600 ambayo ni sawa na Tsh/= 231,770,003.01 na inazidi kupanda.