Timu ya madaktari bingwa imefanikiwa kumfanyia upasuaji Ramadhan Bilali (55), ambaye ni mkazi wa Shinyanga na kuondoa jiwe kwenye kibofu cha mkojo lilolomsumbua kwa miaka sita.
Akizungumza na Jambo Fm, Daktari bingwa wa upasuaji, Dkt. Joachimu Kisaa amesema kuwa upasuaji huo umefanyika katika hospitali ya Ushetu mkoani Shinyanga kupitia kambi ya madaktari bingwa wa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
“Upasuaji huu tumeufanya katika hospitali ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga chini ya madkari bingwa ambao tumeweka kambi ya siku tano hapa halmashauri ya Ushetu,” amesema Dkt. Kisaka.

Ameongoza kuwa mgonjwa huyo amekaa na jiwe hilo kwa zaidi ya miaka sit ana kwamba amezunguka katika hospitali nyingi na kutumia gharama kubwa bila mafanikio.
“Hili tatizo limemsumbua kwa muda mrefu zaidi ya miaka sita,na amesema ametumia gharama kubwa Kwenda katika hospitali mbalimbai bila mafanikio hadi alipokutana na sisi,kwa kwa sasa anaendelea vizuri na afya yake inazidi kuimarika kwa kasi sana,” ameongezea Dkt. Kisana.
Kwa upande wake Ramadhani Bilali amewashukuru madaktari bingwa kwa kumponya ugonjwa uliomtesa kwa muda mrefu bila mafaikio na kwamba kwasasa hali yake inaendelea vizuri huku akiendelea kutumia dawa na kuuguza jeraha.
“Kwa kweli sina cha kuwalipa hawa madaktari Mungu mwenyewe atawalipa, ninawashukuru sana kwa huduma yao nimeteseka kwa muda mrefu sana na hili tatizo ila kwasasa naendelea vizuri kabisa bado natumia dawa na kuuguza kidonda lakini kwa ujumla naendelea vizuri sana,” amesema Bilali.
Madaktari bingwa wa Dkt. Samia Suluhu Hassan wameweka kambi ya siku tano katika hospitali ya Ushetu kuanzia Octoba 13 hadi octoba 17 wakitibu magonjwa ya ndani, magonjwa ya wanawake na uzazi,magonjwa ya ganzi na usingizi, Magonjwa ya watoto wachanga Pamoja na magonjwa ya kinywa na meno.


