Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Miaka sita jela kwa kuiba pikipiki

Watu wawili akiwemo raia wa Burundi, wamehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka sita jela baada ya kukiri kutenda kosa la kuvunja ofisi ya mganga mkuu wa wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza na kuiba pikipiki tatu zenye thamani ya shilingi milioni 11, 850,000.

Akisoma maelezo ya makosa kwa washtakiwa hao, mwendesha mashtaka wa serikali, sajenti wa polisi Theophilius Bei amesema washtakiwa walitenda makosa hayo agosti 20,2023, kwa kuiba pikipiki tatu za serikali kinyume na kanuni ya adhabu sura ya 16 toleo la mwaka 2022.

Katika kesi hiyo yenye washtakiwa watatu, washtakiwa wawili ambao ni Niyokindi Anthony ambae ni mkazi wa Burundi pamoja na Ibrahim Mshengezi mkazi wa wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza wamehukumiwa kwa kutenda makosa mawili ambayo ni kuvunja ofisi na kuiba kinyume na vifungu 297 na 258 vya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2022.

Mshtakiwa mwingine wa kesi hiyo ambaye ni mkazi wa Isungangh’olo wilayani Sengerema, Anold Paul amekana mashtaka hayo ambapo hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama hiyo, Evod Kisoka ameamuru arejeshwe rumande baada ya kukosa wadhamini huku shtaka lake likitarajia kuendelea October 2 mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *