Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Miaka miwili ya Rais Samia, Manyara yapokea Bil. 535.7

Tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani mwaka 2021,mkoa wa Manyara umepokea fedha kiasi cha shilingi bilioni 535.7 zilizotumika katika utelekezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.


Mkuu wa mkoa huo Queen Sendiga amebainisha hayo leo Oktoba 14,2023 katika uwanja wa Tanzanite Babati mkoani Manyara kupitia salamu za mkoa alizozitoa kwa Mh.Rais katika kilele cha mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2023.


Akitoa mfano wa baadhi ya miradi iliyotekekelezwa kupitia fedha hizo Mh.Sendiga ameeleza kwamba kiasi cha bilioni tatu kati ya fedha hizo zinatumika katika ujenzi wa shule maalum ya Sekondari ya wasichana na
kiasi cha shilingi bilioni 5.4 zinazotumika katika ujenzi wa soko la kisasa la madini Mirerani wilayani Simanjiro.


Wakati huo huo mkuu huyo wa mkoa wa Manyara(Queen Sendiga)ameeleza kwamba maadhimisho ya wiki ya vijana kitaifa yaliyoambatana na kumbukizi ya miaka 24 ya kifo cha Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2023 vimechochea ukuaji wa uchumi na utalii kwa mkoa wa Manyara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *