Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Miaka 30 jela kwa kumuingilia kinyume na maumbile mke wake

Boniface Mtweve mkazi wa kata ya Lugarawa Mkoani Njombe amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na Mahakama ya Wilaya ya Ludewa kwa kosa la kumuingilia kinyume na maumbile mke wake ambaye jina lake limehifadhiwa.

Mwendesha mashtaka Asifiwe Asajile mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Isaac Ayeng’o ilielezwa kuwa mwanamke huyo alikwenda kwenye harusi na kuchelewa kurudi nyumbani kwake ambapo aliporejea majira ya usiku alimkuta mumewe nje akimsubiri huku akiwa amekasirika.

Mtuhumiwa huyo alimuamuru mkewe kuingia ndani na alipoingia alianza kumfokea na kumwambia kuwa ametoka kwa wanaume na hakuwa kwenye harusi hivyo anataka amuoneshe kuwa yeye ndiye mwanaume ndani ya nyumbandipo akachukua mafuta na kumfanyia kitendo hicho kitu ambacho ni kinyume cha sheria kifungu namba 154(1) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *