Miaka 30 jela kwa kumbaka mtoto wake

Mkazi wa Kijiji cha Kakola kata ya Bulyanhulu wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga Makungu Juma (41) amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na kulipa faini ya Shilingi laki 500,000 kwa kosa la kumbaka mtoto wake wa kambo Jina linahifadhiwa Mwenye umri wa miaka (12).

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu mkazi wa Mahakama hiyo Christina Chovenye ambapo amesema Mahakama imemtia hatiani Makungu pasipo shaka yeyote kwa kosa hilo la kubaka kinyume na kifungu 130 (1)( 2) (e) na 131 (1) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 Marejeo ya Mwaka 2012.

Amesema upande wa Jamhuri umethibitisha Kosa kwamba Makungu alitenda kosa hilo kwa nyakati tofauti Mwezi Julai hadi Septemba 2023 nyumbani kwake huku akijua wazi kuwa kitendo hicho ni kosa kisheri na atatumikia adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela na kulipa faini ya shilingi laki 5.

Kwa upande wake Wakili wa Serikali Evodia Baimo awali akisoma Shauri hilo la jinai namba 291 la Mwaka huu aliiomba Mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa Makungu ili iwefundisho kwake na kwa watu wengine kwenye jamii wenye tabia kama hiyo.

Kabla ya hukumu hiyo Makungu aliiomba Mahakama hiyo kumpunguzia adhabu hoja ambayo imetupiliwa mbali na tayari ameanza kutumia adhabu hiyo katika Gereza la Wilaya ya kahama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *