Nyota wa filamu ya Fast & Furious, Paul Walker ametimiza miaka 10 tangu afariki kwa ajali akiwa na rafiki yake Roger W. Rodas wakati wawili hao wakiwa ndani ya gari aina ya Porsche Carrera GT.
Ilikuwa mnamo Novemba 30, 2013, wakati Walker na Rodas walifariki huko Valencia, kifo kilichomimina hisia nyingi kwa wapenzi wa filamu na waigizaji wenzake.
“Kaka nitakukumbuka sana. Sina la kusema kabisa,” aliandika mwigizaji mwenza Vin Diesel kwenye ukurasa wake wa Instagram.