MHANDISI JUMBE AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI BAADA YA KURUDISHA FOMU.

NA EUNICE KANUMBA –SHINYANGA 

Katika mwendelezo wa harakati za kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, Kada wa  Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhandisi James Jumbe Wiswa, Julai 2, 2025 alirejesha rasmi fomu ya kuomba ridhaa ya chama chake ili kuwania Ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kurejesha fomu katika Ofisi za CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhandisi Wiswa amesema utaratibu wa kuchukua fomu na urejeshaji umesimamiwa kwa weledi na chama hicho na hapakuwa na malalamiko yeyote. 

 “Leo nimefika kwa mara ya pili. Hatua ya kwanza ilikuwa kuchukua fomu, ambayo niliipokea kwa utaratibu mzuri, nikaijaza kwa uangalifu, na leo nimeirejesha rasmi. Zoezi zima limekuwa la utulivu, la wazi, na bila changamoto yoyote ya kiutendaji,” amesema  Mhandisi Jumbe 

 “Niwapongeze sana viongozi wa CCM wilaya, akiwemo Mwenyekiti, Katibu wa Wilaya, Sekretarieti na watendaji wote kwa maandalizi mazuri. Mchakato umekuwa rahisi na unaoeleweka; unapofika, unapewa control number, unafanya malipo, unachukua fomu, unajaza, na kisha unairejesha bila urasimu,” amesema Jumbe “

Kwa mujibu wa ratiba ya CCM, zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi liliendelea katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani, huku watia nia wakiendelea kujitokeza kwa wingi na mwisho wa zoezi hilo lilikua ni Jana Julai 2 saa kumi kamili jioni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *