Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Mgonjwa wa TB ana uwezo wa kuambukiza watu 20 kwa mwaka

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amewaagiza Wanganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha wanajumuisha huduma za Kifua Kikuu na Ukoma kwenye shughuli zao wanazotekeleza ili kuongeza nguvu za kudhibiti Magonjwa hayo ifikapo Mwaka 2030.

Dkt. Mollel amesema hayo kwenye Mkutano mkuu wa Mwaka wa wataalamu wa Kifua kikuu na Ukoma uliofanyika Mkoani Dar es Salaam huku akisisitiza hatari ya kuambukizwa kwa Zaidi ya watu laki nne kwa mwaka.

Dkt. Mollel amesema kwa takwimu za Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Kifua kikuu na Ukoma, mgonjwa mmoja wa kifua kikuu ambaye hakupata matibabu ana uwezo wa kuambukiza watu 15 hadi 20 kwa mwaka mmoja.

Akieleza mikakati ya kutokomeza Kifua kikuu nchini, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk John Jingu kupitia taarifa yake iliyosomwa na mwakilishi wake Catherine Joachim amesema Tanzania imewekewa lengo na Umoja wa Mataifa kutokomeza maambukizi ya kifua kikuu kufikia 2030

Lengo la kujumuisha magonjwa ya Kifua kikuu na Ukoma kwenye shughuli zinazofanywa na waganga wakuu mikoa na wilaya ni kuendelea kuibua wagonjwa wa kifua kikuu ambao bado hawajaanza tiba

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *