
Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema mgawo wa umeme utamalizika kufikia Machi, 2024 baada ya majaribio ya mtambo namba tisa wa uzalishaji wa umeme katika Bwawa la Mwalimu Nyerere kufanyiwa majaribio jana.
Kapinga amesema hayo leo, Februari 16, 2024 wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Lupembe (CCM), Edwin Swalle aliyehoji taarifa za mitandaoni kuwa leo ingekuwa ni siku ya mwisho wa mgawo wa umeme.
Hata hivyo, Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson ameipa Serikali hadi Juni, 2024 ili usiwe tena na mgawo wa umeme kama alivyoahidi Naibu Waziri, Kapinga.