Mgao wa Umeme endapo mvua zikichelewa

Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Maharage Chande amesema ikiwa mvua za vuli zitachelewa kutakuwa na uhaba wa umeme kutokana na kupungua kwa maji.

Akizungumza katika ziara ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Chande amesema licha ya matumizi ya umeme kuwa makubwa na maji kupungua siku hadi siku Uzalishaji wa umeme bado upo vizuri.

“Vituo vyetu vinafanya kazi ila tusipopata mvua kutakuwa na upungufu wa umeme na kwa sasa tunaomba mvua zinazotegemewa zinyeshe haraka kwa sababu kama hazitanyesha vituo vyetu Vitapata upungufu wa umeme”.

“Kunapokuwa na upungufu wa umeme unatokea mgao, hali hiyo inapotokea huwa tunawaambia wateja wetu kuwa upungu na ndio maana tunasema mvua zisipokuja mapema kutakuwa na upungufu wa umeme,” amesema.

Amesema kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita kumekuwa na kasi ya matumizi ya umeme kwa sababu ya ongezeko la uwekezaji kwenye viwanda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *