Mganga wa kienyeji awalewesha watu 16 na kuwaibia


Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam limesema linachunguza tukio la Mtu mmoja aliyejifanya Mganga wa jadi maeneo ya Mji mwema, Kigamboni aliyewanywesha na kuwalewesha Watu 16 wa Familia moja dawa inayodhaniwa kuwa ni sumu na kisha kuwaibia simu.

Kamanda wa polisi kanda malumu ya Dar Es Salaam Jumanne Muliro amesemaTukio hilo limetokea February 18, 2024 majira ya saa tatu usiku wakati Mtu huyo alipofika nyumbani kwa Familia ya Mzee Halisi Amani kwa lengo la kumtibu Mke wake Fatuma Abdalla (52) aliyekuwa anasumbuliwa na tatizo la miguu ambapo aliwanywesha dawa iliyowalewesha Familia nzima, wakapoteza fahamu na akawaibia simu 5 za mkononi na kuondoka nazo.


Kamanda Muliro ameongeza kuwa Tukio lingine limetokea tarehe 9 Februari, 2024 huko eneo la Tuangoma, Mbagala ambapo Mtu mmoja aliyejifanya Mganga wa jadi aliwanywesha Watu watano dawa zilizowalevya na baadae kupoteza fahamu na kuwaibia pikipiki namba MC474, simu 3 za mkononi na Tsh 30,000, Jeshi la Polisi linawatahadharisha Wananchi kuhusiana na uwepo kwa Watu wanaojifanya waganga wa jadi ambao huwalewesha Watu na wanafamilia kwa ujumla.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *