Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro (DMO), Dk Alex Kazula amekutwa amefariki dunia kwenye nyumba ya kulala wageni ‘gesti’ huku kifo chake kikigubikwa na utata.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kisare Makori amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema mwili wa Dk Kazula ulikutwa Oktoba 9, 2023 kwenye moja ya nyumba za kulala wageni akiwa ameshafariki dunia.
Amesema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama wanachunguza kifo cha daktari huyo ili kujua chanzo chake.
Kwa upande mwingine, Kamanda wa Polisi Mko wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema wanashikiliwa wanawake wawili kwa kukutwa na simu za marehemu.