Mganga aliyembaka  mwanafunzi mbele ya mdogo wake ahukumiwa maisha jela



Mahakama ya Wilaya ya Kigoma, imemhukumu Kalebo Charles (46) ambaye ni mganga wa kienyeji kifungo cha maisha na kuchapwa viboko vitano baada ya kumkuta na hatia ya kumbaka mwanafunzi wa darasa la nne (10) mbele ya mdogo wake.


Akisoma hukumu hiyo hakimu mwandamizi wa Mahakama hiyo, Evelyn Mushi, amesema mtuhumiwa alifanya tukio hilo mnamo mwezi Septemba 03, 2023 ambapo alimchukua mhanga pamoja na mdogo wake na kuwapeleka katika nyumba ya kulala wageni ya Sebabili iliyopo manispaa ya Kigoma ambapo alitekeleza tukio hilo.


Akiongea nje ya mahakama mara baada ya hukumu kutolewa wakili wa serikali, Nestory Kuyula amesema mtuhumiwa alifika nyumbani kwao na muhanga kwa ajili ya kuwasalimia kwani ni familia zinazofahamiana na ndipo alipomwambia mhanga na mdogo wake waongozane nae mahali alipofikia ili mhanga akawaone watoto wa mtuhumiwa na ndipo alipofanya tukio hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *