Taarifa kutokea Kasri ya Kifalme la Uingereza (Buckingham Palace), imeeleza kuwa Mfalme Charles III wa Uingereza amekutwa na ugonjwa wa saratani (Kansa) wakati anapatiwa matibabu ya tezi dume hivi karibuni.
Kasri hiyo imethibitisha kuwa Saratani hiyo si ya tezi dume.
Watu mashuhuri mbalimbali akiwemo Rais Joe Biden wa Marekani wameeleza kushtushwa kwao na taarifa hizi na wamemtakia Mfalme Charles III afya njema.