Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Paul Chacha amemuagiza mkuu wa polisi wilayani humo Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Oscar Mmole kumyanganya bastola Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini (TARURA) wilayani humo, Bright Mndeme ambaye anadaiwa kutishia Wananchi kwa kutumia bastola anayomiliki
Hayo yamejiri baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo Paul Chacha kupokea taarifa kutoka kwa Wananchi juu ya ucheleweshwaji wa barabara ya Nyashishi Fella yenye urefu wa kilomita 8.
Dc Chacha amesema barabara hiyo ilikuwa ikamilike September Mosi mwaka huu lakini mkandarasi alipewa zabuni ya ujenzi wa barabara hiyo hajakamilisha hadi sasa.