Meek Mill asisitiza kuutaka urai wa Ghana


Rapa kutoka nchini Marekani Meek Mill ameeleza nia yake ya kutaka kupata uraia wa Ghana, huku akitaja ukandamizaji wa wanaume weusi, nchini Marekani ndio chanzo cha yeye kutaka kuondoka nchi hiyo.

Msanii huyo mzaliwa wa Philadelphia, ambaye hivi karibuni alikabiliwa na madai ya kuwa na ukaribu wa hatari na rapa Diddy ameeleza hayo kupitia ukurasa wake wa X mnamo Machi 5, 2024.

“Ninataka kupata Uraia wa Ghana, America imetengenezwa kwa ajili ya kuwabomoa Wanaume Weusi kama usipofata maagizo.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *