Mchungaji Mackenzie akutwa na Makosa 191 ya Kujibu

Mahakama nchini Kenya imemkuta na makosa 191 ikiwemo mauaji kiongozi wa kidini anayekabiliwa na utata na washirika wake kwa kuhusishwa na vifo vya karibia watu 200 katika msitu wa Shakahola pwani ya taifa hilo.

Paul Nthenge Mackenzie, ambaye tayari anakabiliwa na mashtaka mengine ikiwemo ugaidi, na kuwatesa watoto, anatuhumiwa kwa kuwashawishi mamia ya wafuasi wake kufunga hadi kufa iliwamuone Yesu.

Mackenzie na washirika wake 29 wamekana mashtaka 191 ya mauaji dhidi yao kwa mujibu wa stakabaadhi za mahakama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *