Mchezo wa Yanga na Azam wasogezwa mbele

Ratiba ya michezo miwili ya Ligi Kuu ya NBC iliyokua ikizikutanisha Yanga Sc, Azam na Singida Fountain Gate imebadilika ili kupisha michuano ya Africa Football League.

Yanga ilipaswa kucheza na Azam Jumapili ya Oktoba 22 ambapo siku hiyo TP Mazembe itakuwa dimbani ikikipiga na Esperance De Tunis katika Dimba la Benjamin Mkapa ikiwa ni mchezo wa kimataifa wa Africa Football League.

Yanga Sc itacheza na Azam Fc, Jumatatu Oktoba 23 kwenye dimba la Azam Complex na itacheza na Singida FG, Oktoba 27, 2023 kwenye Dimba la Benjamin Mkapa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *