Mchezaji wa Timu ya Yanga Dickon Job leo amezindua rasmi kitabu chake kinachozungumzia safari ya maisha yake kwa ujumla, Kupitia ukurasa wake wa Instagram Dickson ameandika ‘Leo ni siku ya kihistoria kwangu✍🏾 Najivunia sana kuwajulisha kuwa kitabu changu cha kwanza, kimezinduliwa rasmi! NIITE DICKSON JOB, Kitabu hiki siyo tu kuhusu soka, bali ni hadithi yangu ya maisha—safari yangu ya kupambana, kushinda vikwazo, na kufanikisha ndoto zangu’ – Job.
‘Nimeandika kitabu hiki na @getrude.mligo kwa ajili yenu, vijana wa Afrika, mnaopambana kila siku kufikia ndoto zenu. Tumeshirikiana na @camarainternational ili kitabu hiki kifike kwenye shule zaidi ya 5000 katika nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Zambia, na Malawi, na kutoa motisha kwa vijana kote Afrika kuamini katika uwezo wao.’ – Job.
‘Kwa wale ambao hampo shule, kitabu kinapatikana ofisi za Divine Destiny Bookstore, Bamaga, opposite na ofisi za Startimes. Na kama unataka kuagiza nakala yako au kujua zaidi, unaweza kuwasiliana nasi kupitia Email: niitedicksonjob@gmail.com au Whatsapp: 0735860264’ – Job
‘Hii ni hadithi yangu, lakini pia ni ya kwenu. Fuateni ndoto zenu, na kumbukeni, hakuna linaloshindikana kwa mtu mwenye juhudi na imani’ – Job.
One response to “MCHEZAJI DICKSON JOB AZINDUA KITABU CHA SAFARI YA MAISHA YAKE…”
musamakasy@gmail.com