Mchengerwa awafunda watumishi

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Mohamed Mchengerwa amesema hatosita kuchukua hatua za kinidhamu kwa watumishi wa sekta ya afya watakaobainika kuzembea katika kuwahudumua wananchi.

Mchengerwa ameyasema hayo leo Oktoba 28, 2023 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa afya ya uzazi na mtoto na viashiria vya malaria Tanzania ya mwaka 2022.

Mbali na hilo Waziri huyo amesema hatafikiria mara mbili kuchukua hatua endapo atabaini kuna uzembe umefanyika kwenye utoaji wa huduma, hivyo ametaka wananchi kutoa taarifa wanapokutana na vitendo visivyofaa kwenye hospitali na vituo vya afya.

Lakini pia amewataka Wakuu wa Mikoa yote Tanzania bara kutopeleka magari ya kubebea wagonjwa waliyokabidhiwa leo kimya kimya bali wajulishe viongozi wa chama Tawala pamoja na wananchi kuwa sasa huduma za usafiri kwa wagonjwa yameongezeka tofauto na hapo awali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *