Mkuu Wa Wilaya Ya Kahama Mkoani Shinyanga, Mboni Mhita Ameanza Kuchukua Hatua Mbalimbali Ya Kukabiliana Na Utoroshaji Wa Madini Ya Dhahabu Unaofanywa Na Baadhi Ya Wafanyabiashara Wasiokuwa Wadilifu Na Kuikosesha Serikali Mapato Yake Yanayotokana Na Madini Hayo.
Hatua Hizo Zimeanza Kuchukuliwa Kuanzia Kwenye Maduara Ya Wachimbaji Wadogo Katika Migodi Yote Midogo, Maeneo Ya Uchenjuaji Wa Madini Pamoja Na Kwenye Masoko Kwa Kujengwa Uzio Ili Kudhibiti Vitendo Hivyo Na Watakaobainika Watawajibishwa Kisheria Ikiwemo Kufutiwa Leseni Zao.
Mhita Ameyabainisha Hayo leo Juni 27, Wakati Wa Ziara Yake Ya Kushtukiza Katika Soko Kuu La Dhahabu Kahama Na Mwime Yaliyopo Halmashauri Ya Manispaa Ya Kahama, Akiambatana Na Kamati Yake Ya Ulinzi Na Usalama Kwa Kushirikiana Na Ofisi Ya Mkoa Wa Kimadini Kahama.
Amesema, Baadhi Ya Wafanyabiashara Wamekuwa Sio Wadilifu Na Wanashirikiana Na Wachimbaji Wadogo Kuibia Serikali Mapato Kwa Kutoa Taarifa Ambazo Sio Sahihi Za Viwango Vya Madini Walivyonavyo Katika Ofisi Za Madini Zilizopo Sokoni Na Wanapokaguliwa Wanakutwa Na Madini Mengi Mfuko.