Makamu Rais, Dkt. Philip Mpango amewataka wakimbiza mwenge wa uhuru mwaka 2025 Kitaifa Kuhakikisha wanafichua vitendo vyote vya ubadhilifu wa fedha za serikali, Rushwa na dhuruma katika mambo yote watakayo yabaini katika miradi ya halmashauri watakayo ipitia katika mbio za Mwenge nchi nzima.
Amesema hayo wakati akihutubia Wananchi katika sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa huko katika viwanja vya Shirika la elimu Kibaha wilayani Kibaha mkoani Pwani.

Amesema wakimbiza Mwenge hao wa Uhuru mwaka 2025 wakafichue vitendo vyote vya ubadhilifu wa fedha za serikali, vitendo vya rushwa, udhalimu na dhuruma kwa Wananchi katika mikoa 31 na Halmshauri 195 nchini.
Makamu pia amezigiza Halmashauri kuwapa ushirikiano wakimbiza mwenge hao wasifiche kuhusu matumizi ya fedha katika miradi ya serikali ilipo kwenye maeneo yao.