Mbaroni kwa kuwalewesha wanawake na kuwadhalilisha kingono

Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar Es Salaam limeendelea kusimamia mifumo ya kuzuia, kubaini na kupambana na vitendo vya kihalifu, ambapo imewanasa

watuhumiwa wa matukio mbalimbali ya uhalifu ambao wanahisiwa kuendesha uhalifu wa kutongoza wanawake, kuwalewesha, kuwadhalilisha kingono, kuwapiga picha, kuwatishia maisha na kisha kuwaibia fedha, simu, laptop na vitu vingine vyenye thamani.

Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar Es Salaam Muliro Jumanne amesema sambamba na watuhumiwa hao wawili ambao uchunguzi wao unaendelea ili kubaini mtandao wao, watuhumiwa wengine waliokamatwa wamekuwa wakijihusisha na uhalifu wa wizi wa simu za mkononi, laptop, luninga, kamera, subwoofer pamoja na makava ya simu aina mbalimbali.

Katika hatua nyingine kamanda muliro amesema jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar Es Salaam limejipanga kuimarisha hali ya usalama kwenye maeneo yote ili wananchi waweze kusherehekea kwa amani na utulivu sikukuu za Krismasi na mwaka mpya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *