Mbaroni kwa kumpa ujauzito mjukuu wake

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia Casto Thomas (55), Mkazi wa Lumba Chini Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro kwa kosa la kumbaka na kumpa mimba mjukuu wake mwenye umri wa miaka 13.

Akithibitisha kuwepo kwa tukio hili, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP Alex Mkama amesema amekamatwa kwa kumfanyia mjukuu wake vitendo vya ukatili na kukatisha ndoto zake za kuendelea na elimu.

Amesema kukamatwa kwa mzee huyo ni matokeo ya uelewa na utambuzi wa wananchi, ambao walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi baada ya kubaini mtoto huyo kuwa na ujauzito.

Kwa mujibu wa Kamanda Mkama, Casto Thomas atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili baada ya uchunguzi kukamilika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *