Mbaroni kwa kuiba ng’ombe wa Rais

Watu watatu akiwemo mfanyakazi wa shamba la mifugo la serikali Mabuki lililopo katika wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza wanashikiliwa na jeshi la polisi wilayani humo kwa tuhuma za wizi wa ngombe tisa za mradi wa kuwezesha vijana BBT.

Akizungumzia tukio hilo mkuu wa wilaya ya Misungwi Ya Paul Chacha amesema watuhumiwa hao ni Daud Msobi, Shileta Paul, pamoja na Boniphace Kileleju ambao waliiba ngombe hao katika shamba hilo na mara baada ya kuwaiba walikwenda kuwauza kwa mnunuzi ambae bado jeshi la polisi linaendelea kumtafuta.

Kwa upande wake meneja wa mradi huo Jackob Chacha amesema zoezi la kuwakamata watuhumiwa hao limekuja mara baada ya kuonekana kuna upungufu wa ngombe waliokuwepo katika mradi huo ndipo uchunguzi ulipofanyika na kubaini watuhumiwa hao ambao wote wamekiri kufanya tukio hilo.

Nae katibu tawala wa wilaya hiyo Abdi Makange amesema rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hasani alitoa ngombe 950 katika wilaya hiyo ikiwa ni sehemu ya vijana kujiajiri hivyo wao kama viongozi hawako tayari kuona mtumishi yoyote anashiriki katika kuhujumu mradi huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *