Waziri wa uchukuzi Profesa Makame Mbarawa Ametoa maagizo kwa mamlaka ya hali ya hewa nchini kukamilisha kwa haraka ujenzi wa vituo vya kupimia Hali ya hewa (Rada) Ili Wananchi waweze kupata taarifa za uhakika kwa haraka na kuweza kudhibiti baadhi ya majanga.

Profesa Mbarawa ametoa maagizo hayo akiwa Jijini Mbeya alipotembelea na kukagua kituo cha Rada kinachojengwa eneo la Kawetele kitakachoweza kupima Mikoa mitano ya kanda za Nyanda za juu Kusini.
Nae mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini Oran Njeza na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya wameipongeza mamlaka ya hali ya hewa kwa kutoa taarifa sahihi ikiwemo za athari za mafuriko yanatotokea Hali inayowapa utayari Wananchi na kuchukua tahadhali