Bondia wa zamani wa kulipwa Floyd Mayweather ameweka wazi kutumia kiasi cha dola milioni 1.13 sawa na TZS Bilioni 2.9 kununua Suite Ticket ili kuangalia fainali ya Super Bowl LVIII, siku ya Jumapili hii huko Las Vegas, Nevada.
Bondia huyo ataungana na watu wengine 34 kwenye Suit Ticket kushuhudia fainali za ubingwa wa NFL kati ya Kansas City Chiefs na San Francisco 49ers katika Uwanja wa Allegiant.
Kwa upande wa burudani mwaka huu kwenye uper Bowl Half Time Msanii Usher Raynond ndiye anaetarajiwa kuwapa furaha mashabiki watakaojitokeza kutazama fainali hizo.