Mavunde awafikia Geita Gold FC atoa miezi 6

Waziri wa Madini Antony Mavundeamewataka viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Geita kuhakikisha ndani ya miezi 6 wanasimamia ipasavyo kukamilishwa kwa ujezi wa uwanja wa Magogo wenye uwezo wa kubeba mashabiki elfu 20 ambao utatumiwa na timu ya Geita Gold Fc inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mavunde ameyasema hayo leo Octoba 13 2023 wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Basi jipya kwa timu ya Geita Gold Fc iliyofanyika katika viwanja vya Soko Kuu la Dhahabu Mkoani Geita ambapo amesema viongozi kwa kushirikiana na Mdhamini wa timu hiyo Mgodi wa GGML Wahakikishe Ujenzi wa uwanja huo ukamilike ndani ya miezi sita ili kuwaondolea adha mashabaiki wa timu hiyo kushudia mechi za Simba na Yanga Mkoani Geita Mwanza.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela amewataka wachezaji wa timu hiyo kutokubweteka na usafiri huo uliotolewa na mdhamini Mkuu Mgodi wa GGML na badala yake iwe chachu ya kuchochea matokeo mazuri na kujituma kwa wachezaji hao kwani wao ndo wamebeba dhamana ya wakazi wa Geita kuleta mafanikio makubwa ya kisoka Mkoani humo.

Mkurugezi wa Mgodi wa GGML Terry Strong ambao ni wadhamini wa wakuu wa Timu hiyo amesema wataendelea kuisaidia timu ya GGF ili kuhakikisha inafanya vizuri kwenye michezo yake ili kuleta tija katika jamii.

Katibu Mkuu wa Geita Gold FC Simon Shija amesema changamoto kubwa iliyokuwa inawakabili GGFC katika uendeshaji wake ilikuwa ni usafiri kwa klabu hiyo na sasa changamoto hiyo imetatuliwa hivyo amewapongeza wadhamini wao wakuu na sasa usafiri huo utaisadia timu hiyo kuongeza ushindani ndani ya ligi Kuu Tanzania bara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *