Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Matumizi haba ya vyoo chanzo cha ugonjwa wa kichocho

Tabia ya kuogelea katika mabwawa na madimbwi pamoja na matumizi haba ya vyoo ni miongoni mwa sababu zianazopelekea uwepo wa magonjwa ya minyoo ya tumbo na kichocho kwa watoto Mkoani Shinyanga.

Mratibu wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele mkoa wa Shinyanga Timothy Ruben Sosoma amebainisha hayo wakati akizungumza kando ya kikao cha uraghabishi kwaajili ya maandalizi ya kampeni ya kutoa dawa za minyoo ya tumbo na kichocho kwa watoto wenye umri wa miaka 5-14 na kutumia fursa hiyo kusisitiza matumizi ya vyoo.

Kupitia Kampeni ya Utoaji kingatiba inayotarajiwa kufanyika siku moja kwa mkoa mzima ambayo ni Novemba 24,mwaka huu watoto 286,782 watapatiwa dawa za kichocho na watoto 466,095 watapatiwa dawa za minyoo ya tumbo.

Awali akizungumza kuhusiana na usalama wa kingatiba hiyo, mkuu wa wa mkoa wa Shinyanga Christine Mndeme amesema dawa hizo hazina madhara kwa mtoto yeyote bali ni kinga nzuri wa watoto watakaopatiwa.

Januari 27,2022 Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan alisaini azimio la Kigali lenye lengo la kuhakikisha Tanzania inajitoa kwa asilimia 100 katika kuhakikisha inatokomeza magonjwa ya kichocho na minyoo ya tumbo ifikapo mwaka 2030.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *