Frank Aman – Geita.
Wananchi wa Kata ya Bukoli katika Manispaa ya Geita wameelezea Matumaini yao yatakayo wawezesha kupata Maendeleo na kuboresha hali ya Uchumi wa Mkoa huo kufuatia kupandishwa hadhi kwa Halmashauri ya Mji wa Geita na kuwa Manispaa.
Pia wameelezea namna Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Samia Suluhu Hassan ilivyofanikisha ujenzi wa Shule za Sekondari zaidi ya 150 katika kipindi kifupi cha Uongozi wake.
Kufuatia Maamuzi hayo, Baadhi ya Viongozi na Wananchi wa Halmashauri hiyo wameridhishwa na kuupongeza uamuzi wa Rais Samia na kusema kuwa matumani yao mara baada ya kupandishwa hadhi kwa Halmahauri hiyo ni kuongezeka kwa Huduma muhimu za Kijamii ikiwemo Shule na Hospitali.
Pia huduma zingine muhimu kama Maji, Barabara na Miundombinu mingine iendelee kuboreshwa ili kuipa hadhi Manispaa hiyo na kuwawezesha kuendelea na Shughuli zao za Kila Siku bila kuwepo na Changamoto yoyote.
Nassor Juma ambaye ni Afisa Mtendaji Kata ya Bukoli ameelezea kuwa Maamuzi hayo pia yatakuwa na manufaa kwa eneo lake ambapo Sasa katika Zahanati ya Kata hiyo wanategemea kuongezeka kwa Huduma muhimu za Afya ikiwemo za Upasuaji na Huduma za Mama na Mtoto katika Hospitali iliyopo katika Kata hiyo.
Akitoa Taarifa ya Shughuli za Maendeleo katika Halmashauri hiyo, Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Lucy Beda amesema kuwa katika kipindi cha Miaka Minne ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan wameweza kukamilisha ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto na Zahanati ya Kijiji cha Bugogo, ujenzi uliogharimu kiasi cha Sh400 Milioni ambapo umefikia Asilimia 98 kukamilika.
Akizungumzia Hilo, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigela amesema kuwa utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo hiyo ikiwemo ya ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto na Zahanati ya Kijiji katika Kata ya Bugogo utasaidia katika kuboresha Huduma za kujifungua na kuongeza ufanisi wa Watumishi wa Sekta hizo, hususani kwa Watoto walio na changamoto.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashim Komba amesema kuwa hadi sasa wamepokea kiasi cha Sh500 Milioni kumalizia Wodi mbili katika Hospitali ya Wilaya iliyoko Katoro na ujenzi wa Nyumba moja ya Mtumishi.