Matope yawakimbiza wateja

Wafanyabiashara wa soko la matunda Mirongo lililopo jijini Mwanza wameiomba serikali iweze kufanya maboresho ya miundombinu ya njia za kupita katika soko hilo hii ni baada ya soko hilo kujaa matope yanayosababishwa na mvua zinazoendelea hali ambayo inapelekea kukosekana kwa wateja.

Wakizungumza na Jambo Fm wafanyabiashara wa soko hilo wamesema hali ya biashara kwa sasa ni ngumu hii ni kutokana na kukosekana kwa wateja katika kipindi hiki cha mvua kwani kumekua na wingi wa matope ambayo yamekuwa kero kubwa wakati wa kupita.

Wafanyabiashara hao pia wamesema hali ya usafi katika soko hilo bado nayo sio ya kuridhisha sana hivyo maboresho makubwa yanatakiwa kufanyika ili wananchi waweze kupata huduma bora katika mazingira yaliyo mazuri.

Kwa upande wake mwenyekiti wa soko hilo Alex Mbilingi amesema ili kukabiliana na changamoto ya uchafu katika soko tayari wameshazungumza na wafanyabiashara wa eneo hilo na kumtaka kila mmja awe na chombo cha kuhifadhia uchafu na katika suala la miundombinu wao kama uongozi wanakwenda kufanya kikao na wafanyabiashara wa siko hilo ili kuona ni namna gani ya kutatua changamoto hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *