Mwaka 2024 ndio ambao tupo kwa sasa na ikiwa bado ni Januari mastaa wa Nchini wanatumia muda huu kushare nasi mijengo yao wanayomiliki kwa sasa.
Wiki moja iliyopita staa wa filamu Jackline Wolper alishare nasi video ya mjengo wake ambao alikuwa akijenga na sasa umekamilika na ataweza kuishi na familia yake.
Na Januari 3, DJ Ally B alitumia ukurasa wake wa Instagram kushare nasi mjengo wake mpya ambao unafanyiwa marekebishao na jana (Januari 4) mwanamitandao Mwijaku alionesha video za mjengo wa ndoto zake ambao upo Kigamboni unaozidiliwa leo ambao anafungua nao mwaka 2024.