Mastaa waliokiwasha matamasha ya michezo

Soko la muziki wa Afrobeat linazidi kukuwa huku mastaa wa Afrika wakikiwasha vilivyo kwenye matamasha makubwa ya michezo Dunia.


Utakumbuka mwaka 2019 staa kutoka Tanzania Daimond Platnumz, alikiwasha kwenye tuzo za CAF,zilizofanyika nchini Misri.


Mwingine ni Davido, yeye amekiwasha kwenye fainali za Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar. Desemba 18.


Pia Burna Boy yeye amekinukisha kwenye NBA All-Star half time akiwa na Rema pamoja na Tems mwezi Febuari mwaka huu na Juni 11 pia alitumbuiza
kwenye UEFA Champions League, huko Istanbul nchini Uturuki.



Na Oktoba 20 mwaka huu kutoka hapa 255, Alikiba alikisanua kwenye ufunguzi wa African Football Leauge inayohusisha vilabu vikubwa Afrika vinavyofanya vizuri.

Na hivi karibuni Rema amekinukisha kwenye Ballon D’or iliyofanyi hivi juzi nchini Ufaransa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *