MASTAA WAANZA KUTUA TANZANIA

Nyota wa zamani wa Ajax, PSG, AC Milan, Barcelona na Manchester United, Zlatan Ibrahimovic ambaye kwa sasa ni sehemu ya washauri katika uongozi wa mabingwa mara 7 wa Uefa miamba AC Milan, yupo Tanzania

Zlatan nyota pia aliyepata kuiongza Timu ya Taifa ya Sweeden amepost akiwa eneo la Kogatende kwenye Hifadhi ya Taifa ya Serengeti nchini Tanzania; kitovu cha uhamaji wa wanyama maelfu wanaovuka Mto Mara.

Kwa mujibu wa wataalam, eneo la Kogatende ndiko ambako mwezi kama huu wa Juni wanyama wengi hasa nyumbu hujaa huko wakiwa tayari kufanya lile tukio mashuhuri kwa sasa duniani la kuvuka mto Mara (World’s Biggest Wildebeest Migration).

“Wengi wanakuja na Agosti kuna ‘breaking news’ kubwa kuhusu mastaa na utalii wa Tanzania,” anasema mmoja wa mawakala wakubwa wa utalii nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *