Miaka ya hivi karibuni wimbi la washona suti za kiume limekuwa kubwa sana hii ni kutokana na watu wengi kutaka kuonekana nadhifu na wanaovutia ila pia bei sio zile za kuumiza sana. Yani fundi A akisema milioni unaenda kwa fundi B yeye anafanya nusu yake au hata robo.

Ila raha ya kuvalia suti lazima uwe na mwili flani ambao hauna kitambi sana na pia ujue rangi nzuri za kitambaa cha suti zitakazoendana na mwili wako.
Na hawa ndio baadhi ya mastaa wa Bongo wanaopendeza wakivalia Suti:- Ommy Dimpozi, Jux,Harmonize, Diamond Platnumz, Marioo, MC Gara B, Calisa, Izzo Biznes, Barnaba, Tommy Flavor.

Pia kuna Dickson Job, Gadiel Michael, Quick Rocka, Kusah,Ibrah, K2ga, Alikiba, G Nako, Manula na wengineo ambao unawajua ila hapa tumeshindwa kuwataja.


